HabariPilipili FmPilipili FM News

Inspeka Generali Aamrisha Uchunguzi Kufanyiwa Kuhusu Kisa Cha Kutiwa Mbaroni Kwa Wanahabari Wa Shrika La Nation.

Inspekta generali wa polisi Joseph Boinett ameamuru uchunguzi kufanywa kufuatia kisa ambapo wanahabari watatu wa shirika la habari la Nation walinyanyaswa walipokuwa kazini huko Shanzu jana adhuhuri.

Inadaiwa walivamiwa na kundi la watu wanaokisiwa kuwa maafisa wa polisi kabla ya kutiwa mbaroni wakati wakipiga picha kuhusu masuala ya utalii karibu na hoteli moja inayojengwa eneo la shanzu.

Wanahabari hao hata hivyo waliachiliwa baadae baada ya kamanda wa polisi kaunti ya momba Johnstone Ipara kuingilia kati.

Show More

Related Articles