HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Wahimizwa Kujiunga Na Vya Kiufundi Kwale.

Gavana wa kaunti ya  Kwale Salim Mvurya amewahimiza  vijana ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na Vyuo Vikuu wajiunge na vyuo vya ufundi ili wapate taaluma zitakazo waendeleza maishani.

Mvurya amekariri kwamba Serikali ya Kaunti imeipa kipaumbele suala la elimu ili kuhakikisha jamii ya Kwale inaendelea akisema kwamba  kila mwanafunzi anayejiunga na Chuo cha Ufundi  Kwale analipiwa shilingi elfu 15 na Serikali ya Kaunti

Kando na hayo Gavana Mvurya  amedokeza kuhusu kujitolea kwa Serikali ya Kaunti kuhakikisha wakazi wa Kwale wanapata huduma bora za matibabu, maji safi sambamba na kuimarisha miundo msingi mashinani.

Show More

Related Articles