HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Kutoka Eneo La Pwani Waafikiana Kufufua Jumuiya Ya Kaunti Za Pwani.

Mabunge ya kaunti za pwani yamekubaliana kwa kauli moja kufufua mpango wa Jumuiya Ya Kaunti Za Pwani, hiyo ikiwa njia mojawapo ya kuwasilisha ajenda na matakwa ya wakazi wapwani.

Kupitia msemaji wa jumuiya hiyo James Dawa aliye pia mwakilishi wa wadi ya Puma huko Kinango, mabunge ya pwani sasa yameipa Jumuia ya kaunti ya pwani majukumu matatu muhimu, ikiwemo kuangazia matatizo ya ardhi, umiliki wa bandari ya Mombasa na kuleta viongozi wote wa pwani pamoja.

Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho amesema kwa sasa hakuna mgawanyiko wowote miongoni mwa viongozi eneo hili la pwani.

Show More

Related Articles