HabariMilele FmSwahili

Wawakilishi wa wadi Homabay watofautiana kuhusu madai ya kupokea hongo ili kupasisha bajeti  ya kaunti.

Wawakilishi wa wadi kaunti ya Homabay wametofautiana kuhusu madai ya kupokea hongo ya shilingi milioni 3 ili kupasisha bajeti  ya kaunti.Mwakilishi wa wadi ya Ruma Kaksingri Eliphalet Osuri Omoro amekana na kulitenga bunge hilo na madai hayo huku akiyataja kama uvumi unaolenga kulipaka tope na kwamba yupo tayari kujiuzulu iwapo alihusika alipokea pesa hizo hoja iliyoungwa mkono na Maurice Ogwang wa wadi ya Kendu Town.Mwakilishi mteule na ambaye pia ni kiranja wa wengi Sophy Koweje ameeleza jinsi mwakilishi wadi wa Karachuonyo Central Julius Odhaimbo Gaya  alivyowaelezea mahali na jina la mkahawa ambapo wangekutana ili wapokee hongo hiyo na   kuwa serikali ya kaunti ilitoa pendekezo la shilingi nusu milioni offa ambayo ilikataliwa na wawakilishi wadi waliochaguliwa.

Show More

Related Articles