HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Nairobi Yaongoza Kwa Idadi Ya Wanafunzi Ambao Huacha Shule.

Kaunti tisa humu nchini zimetajwa kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambao huacha shule za msingi.

Kaunti hizo ni pamoja na Nairobi,Wajir,Turkana,Mandera,Tanariver,Garisa,Idiolo,Marsabit na Pokot magharibi.

Akizungumza alipokua anahutubia walimu wakuu katika kongamano la KEPSHA,mkurugenzi mkuu wa elimu ya shule za msingi Abdi Habat amesema sababu kuu ya wanafunzi kutomaliza shule ni pamoja na umaskini,ukame,ndoa za mapema na tamaduni potofu katika jamii kama vile ukeketaji.

Habat ameongeza kuwa takriban wanafunzi laki nane na elfu hamsini wameacha shule kutoka mwaka 2016 hadi mwaka huu huku wengi wao wakiwa wanafunzi wenye ulemavu.

Show More

Related Articles