HabariMilele FmSwahili

Mwanamke mmoja ajehuriwa baada ya kumwagiwa maji moto na mumewe Gatundu Kaskazini

Mwanamke mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kumwagiwa maji moto na mumewe katika kijiji cha  Kanjuku Gatundu kaskazini. Kulingana na majirani Samuel Nguta Kanunu amekuwa akizozana na mkewe Anne njeri kwa muda mrefu. Aidha Nguta anaarifiwa kuteketeza nyumba yao kwa kutumia petroli kabla ya majirani kumwokoa mkewe. Mke huyo anauguza majeraha katika hospitali ya Igegania Level 4. Chifu wa eneo la Gathaiti ,Joshua Kung’u ameshutumu vikali tukio hilo na kusema mume huyo aliyetoroka anasakwa.

Show More

Related Articles