HabariMilele FmSwahili

Atwoli ataka wabunge waliopokea hongo kuangusha ripoti ya sukari kuchukuliwa hatua

Shinikizo linazidi kutolewa kwa bunge kuwachukulia hatua wabunge waliodaiwa kupokea hongo ili kuiangisha ripoti ya kuhusu uchunguzi wa sukari. Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli anasema wabunge wote waliotajwa katika uovu huo hawapaswi kusazwa. Amemtaka kiongozi wa wachache bungeni John mbadi kuwajibikia madai kuwa alihongwa ili kuwalinda walaghai walioagiza sukari hiyo. Aidha Atwolli ameitaka serikali kuwachukulia hatua maafisa wa hazina ya malipo ya uzeeni NSSF kwa kuhusika katika ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya afisi. Amedai kuwa na ushahidi kuhusiana na madai ya ufisadi katika NSSF mwaka wa 2014. Kadhalika muungano wa COTU umetetea hatua ya kubomoa majengo yaliyomo katika mikondo ya mito hapa jijini na kusema unapaswa kutekelezwa kikamilifu.

Show More

Related Articles