HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Taita Taveta Yakumbwa Na Ukosefu Wa Fedha.

Licha ya kaunti ya Taita Taveta kuwa mojawapo ya kaunti zilizo na vivutio mbali mbali vya utalii jambo ambalo lingeiwezesha kukusanya fedha za kutosha kuimarisha sekta ya utalii, sasa wizara husika kwenye kaunti hiyo imesema haina fedha za kutosha  kufanikisha agenda yake.

Katibu wa utalii kaunti hiyo Getrude Shuwe anasema hali hiyo imewasukuma kutafuta wadau na wahisani mbali mbali kwenye sekta hiyo ili kujiimarisha  ili kuingia kwenye mikataba ya maelewano nao.

Katibu huyo kadhalika amesema pia wizara hiyo inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi ambapo imembidi kuomba usaidizi kutoka kwa wizara zingine.

Show More

Related Articles