Mediamax Network Limited

K’ogalo wanusia kombe

Baada ya kuichabanga Kakamega Homeboyz hapo jana magoli 3-1 , mabingwa watetezi wa ligi kuu KPL waite Gor Mahia wanahitaji pointi tisa tu , yani kushinda mechi tatu kati ya tisa walizosalia nazo msimu huu kutawazwa mabingwa .Siku ya alhamisi Kogalo wanakutana na Chemelil mechi ya ligi kuu KPL kabla ya kugaragazana na Rayon Sport mtanange wa CAF siku ya jumapili . Watakutana na batoto ba mungu Sofapaka tarehe 22 mwezi huu , kisha wazame kwenye dabi la mashemeji dhidi ya AFC Leopards tarehe 25 . Gor mahia watamaliza mwezi huu wa agosti kwa kusafiri Algeria kukwangurana na USMA Algiers tarehe 29 .