Mediamax Network Limited

Kwanthanze walenga kung’aa zaidi mashindano ya shule za upili

Mashindano ya shule za upili muhula wa pili kitengo cha Afrika mashariki yameingia siku ya tatu hii leo na wawakilishi wa kenya kwenye voliboli ya akina dada Kwanthanze wanalenga kung’aa zaidi baada ya kuanza mashindano hayo kwa ushindi .Hapo jana Kwanthanze iliipiga ST.Alloys ya Rwanda seti  3-2 (17-25,25-19,21-25,25-18,15-8) kwenye mechi ya ufunguzi .Hii leo wanakutana na na IPRC Kigali ya Rwanda na kocha wa vipusa hao Justine Kigwari anasema lengo lao kuu ni wamalize kileleni mwa kundi B . Ushindi hii leo utawapa nafasi nzuri ya kufuzu awamu ifuatayo .