HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao Walalamikia Kunyimwa Huduma Bora Za Kiafya.

Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao wanalalamikia hudumu duni katika hsopitali pale wanapokwenda kutafuta matibabu endapo wameathirika na magonjwa ya STI.

Kulingana na Vincent Ksavery kutoka shirika la PEMA Kenya Trust, wengi wao wanaendelea kuumia na magonjwa ya zinaa kwani hawapati huduma zinazohitajika kufuatia ukosefu wa taaluma ya kuwatibu kutoka kwa wahudumu wa afya.

Wakati huo huo amesema wao kama PEMA wakishirikiana na NASCOP na LGBT wameanzisha mpango maalum wa kuwapatia mafunzo wahudumu wa fya katika hospitali 15 hapa Mombasa ili angalau wasaidike wanapofika hospitalini kutafuta huduma muhimu.

Show More

Related Articles