HabariMilele FmSwahili

Tume ya kitaifa ya ardhi kuandaa mkao wa  dharura leo

Tume ya kitaifa ya ardhi itaandaa mkao wa dharura leo kujadili mwelekeo wake kufuatia kushtwakiwa mwenyekiti Dkt Mohamed Swazuri kwa tuhuma za ufisadi. Mahakama jana ilimwagiza Swazuri na maafisa wengine wa NLC wanaokabiliwa na kesi ya ufisadi kutofika katika afisi zao kesi hii ikiendelea. Jaji Lawrence Mugambi alisema iwapo watanuia kufika afisini watahitajika kuandamana na afisa wa polisi. Swazuri na wenzake wanadaiwa kufuja shilingi milioni 221 za kununua ardhi ya umma kwa ujenzi wa SGR eneo la Embakasi.Swazuri alikana madai hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3.5 pesa taslimu au bondi ya milioni 6.

Show More

Related Articles