HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Swazuri na washukiwa 5 waachiliwa kwa dhamana ya milioni 3.5 pesa taslimu

Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi Mohammed Swazuri pamoja na washukiwa wengine watano wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3.5 pesa taslimu au dhamana ya shilingi milioni 6 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho baada ya kukanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yao.

Washukiwa wengine 12 akiwemo Meneja Mkurugenzi wa shirika la Reli Atanas Maina nao pia wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1.5 pesa taslimu au dhamana ya shilingi milioni tatu na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Show More

Related Articles