HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Katika Kaunti Ya Kwale Waombwa Kujiepusha Na Makundi Ya Uhalifu.

Wito umetolewa kwa vijana kaunti ya Kwale kujiepusha na makundi yenye misimamo mikali  ya kigaidi na badala yake wazingatie masomo ili waweze kupambana na umaskini katika jamii ili kuhakikisha maendeleo na uimarikaji wa uchumi katika kaunti hiyo.

Zainabu Chitsangi   ambaye ni mwanzilishi wa  wakfu wa Zainabu Chitsangi Kwale aliyekua akizungumza na wanahabari katika kongamano la vijana lililofanyika katika ukumbi wa kitamaduni mjini Kwale  amesema kwa kipindi kirefu vijana katika kaunti hio wamekua wakihusishwa na visa vya kigaidi hatua iliyofanya baadhi yao kupoteza maisha  yao kiholela pasi na hatia.

Chitsangi  akiwataka vijana wanaomaliza kidato cha nne na darasa la nane kukumbatia vyema ufadhili wa  masomo unaotolewa na serikali  ya kaunti ya kwale pamoja na mashirika mbalimbali ili kuona kuwa wanaafikia ndoto zao za maendeleo.

Show More

Related Articles