HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Watahadharishwa Dhidi Ya “slay Queens”, Mombasa.

Zaidi ya walimu wakuu elfu 10  wanaohudhuria kongamano la walimu la KEPSHA hapa Mombasa wametahadharishwa kuwa waangalifu wasilaghaiwe  na  vidosho wanaofahamika kama Slay queen.

Naibu kamishena katika gatuzi dogo la Kisauni Kipchumba Ruto, amesema vidosho wengi watakuwa wakiwanyemelea walimu hao kwa lengo wa kuwapora pesa, hivyo basi wanafaa kuwa waangalifu licha ya vitengo vya usalama kuwahakikishia usalama wa kutosha.

Show More

Related Articles