HabariMilele FmSwahili

Kongamano la walimu wakuu wa shule za msingi kuanza rasmi huko Mombasa leo

Kongamano la walimu wakuu wa shule za msingi linaanza rasmi huko Mombasa hivi leo. Zaidi ya walimu wakuu 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo kuangazia hatua ambazo zimepigwa katika elimu ya msingi na changamoto zinazokabili sekta ya elimu nchini. Kongamano hilo pia litatumiwa kujadili mtaala mpya na mafanikio yake, kuajiriwa walimu maeneo wanakotoka na pia kutwaliwa ardhi za shule.

Show More

Related Articles