HabariK24 TvSwahiliVideos

NGARIBA WA TIBA : Baadhi ya wauguzi wahusika katika kuwakeketa wasichana kaunti ya Marsabit

NGARIBA WA TIBA

Jamii nyingi  zimegeukia wahudumu wa afya  kutekeleza ukeketaji wa wasichana,wengi wakisema kuwa ni  njia  moja ya kupunguza madhara ya ukeketaji huku wakidumisha tamaduni zao.mbinu nyingine ikiwa ni watu wa jamii  za Borana katika kaunti ya Marasabit kuwapeleka binti zao nchi jirani ya Ethiopia kupashwa tohara.

 Basi mamia ya wasichana wamesalia mateka wa tamaduni ya  kukeketaji huku familia zao zikiendelea kujitetea kuwa  namna wanayotekeleza tamaduni hii iliyopitwa  na  wakati  haiana  madhara.

 Mwanahabari wetu Nancy Onyancha alizuru kaunti ya Marasabit na kutuandalia  taarifa hii kuhusu masaibu yanayowakumba wasichana wa jamii ya Borana  katika kaunti hiyo na juhudi za kumaliza  tamaduni hiyo.

 

Show More

Related Articles