HabariMilele FmSwahili

Rais atakiwa kubuni jopo kuchunguza sukari bandia nchini

Rais Uhuru Kenyatta ametakiwa kubuni jopo maalum litakaloendesha uchunguzi kuhusiana na sukari bandia nchini. Ni baada ya bunge kutupilia mbali ripoti ya uchunguzi wa sukari hiyo, mbunge wa Kiminini Didmus Barasa akidai wabunge walipewa hongo ili kuwanusuru mawaziri Henry Rotich na Adan Mohammed. Akiongea huko Bungoma leo, amesema jopo hilo linafaa kubuniwa haraka kufichua ukweli kuhusu sakata hiyo.

Naye mbunge wa Saboti Caleb Hamisi amewataka mawaziri kuwajibika na kujiondoa katika nafasi hizo kuruhusu uchunguzi.

Show More

Related Articles