HabariMilele FmSwahili

Mwenyekiti wa tume ya Ardhi Mohammed Swazuri akamatwa

Mwenyekiti wa tume ya Ardhi Mohammed Swazuri, afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Tom Chavangi na mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Athanas Maina ni miongoni mwa watu wengine saba ambao watashtakiwa kwa kupokea hongo wakati wa kuwafidia waliohamishwa kutoka ardhi zao, ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa, SGR .Wote hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu baada ya afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajj kudhinisha hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao. Swazuri anadaiwa kuitisha hongo ya zaidi ya shilingi milioni moja ili kuharakisha shughuli ya kumfidia mmoja wa walioathiriwa na mradi huo wa SGR.

Show More

Related Articles