HabariPilipili FmPilipili FM News

Mawaziri Waambiwa Kuwacha Uwoga Wakufika Mbele Ya Bunge.

Mbunge wa Suna Mashariki junet Mohamed amehimiza mawaziri wawe wakiitikia mwito wakufika bungeni kuhojiwa wanapohitajika.

Akiongea katika kikao kilicho wajumuisha spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi pamoja na  wenyekiti wa kamati mbali mbali za bunge Junet amewalaumu mawaziri ambao hukaidi kufika mbele ya bunge kuhojiwa kuhusiana na utendajikazi akisema ni jukumu la bunge kuwanyoosha mawaziri wanaozembea kwenye kazi zao za uwaziri.

 Naye spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi ameonekana kuwatetea mawaziri akisema wengi wao hawana uzoefu wa kisiasa na huogopa kufika bungeni kujitetea wanapohitajika huku akiongezea kunahitajika uhamasishaji zaidi kuhusu swala hilo la mawaziri kufika bungeni kujitetea kwani wengine huogopa hatakufika mbele ya kamati za bunge.

Show More

Related Articles