MakalaPilipili FmPilipili FM News

Bangi Ya Thamani Ya Nusu Milioni Yanaswa Voi.

Polisi mjini Voi wamenasa misokoto 2,140 ya bangi ya thamani ya nusu milioni iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea Mombasa kutoka Nairobi.

Kulingana na Ocpd wa eneo la Voi Joseph Chesire,bangi hiyo imenaswa eneo la Ndara barabara kuu ya Nrb-Msa wakati polisi wakiendelea na operesheni yao ya kila siku.

Dereva wa lori lililokuwa likisafirisha bangi hiyo anazuliwa katika kituo cha polisi mjini Voi akisubiri kufikishwa mahakamani leo huku uchunguzi ukiendelezwa kubaini wahusika wa biashara hiyo ikizingatiwa dereva huyo amesema amepewa kazi ya kusafirisha mzigo huo hadi Mombasa.

Show More

Related Articles