HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Kitui yaomboleza wanafunzi 10 walioangamia ajalini kwa misa ya wafu

Serikali imewataka walimu na wazazi kushirikiana kudhamini na kuwahakikishia wanafunzi usalama hasa wanaposafiri ili kuepuka maafa yatokanayo na ajali barabarani.

Himizo hilo limetolewa mjini Mwingi kaunti ya Kitui kwenye misa ya wafu iliyoandaliwa katika uwanja wa St. Joseph seminary grounds.

Familia za wanafunzi kumi wa shule ya msingi ya St. Gabriel walioangamia kwenye ajali walipokuwa wakirejea makwao kutoka ziara ya masomo jijini Mombasa zilifarijiwa.

Waziri wa Elimu Amina Mohammed alisoma hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta huku akiandamana na viongozi wengi.

Show More

Related Articles