HabariMilele FmSwahili

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Kidero akana madai ya ufisadi dhidi yake

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero amekana mashtaka ya matumizi mabaya ya pesa za kaunti na kupokea fedha kwa njia za ulaghai. Kidero ambaye alifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya ufisadi Douglas Ogoti pamoja na aliyekuwa afisa wa fedha kaitka kaunti yake Maurice Ochieng Okello, anatuhumiwa kuhusika katika ubadhirifu wa shilingi milioni 213 pesa za kaunti ya Mairobi miongoni mwa madai mengine yanayohusu kupokea fedha kutoka Lodwar Wholesalers kwa njia tatanishi kati ya mwaka 2014-2016. Awali wakili Tom Ojienda alilalamikia kuzuiliwa mteja wake bila dhamama akidai EACC ilikiuka haki zake.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Alexander Muteti umepuzilia mbali madai hayo.Hakimu Ogoti hata hivyo ameagiza kuwa kesi zote za ufisadi zitakazowasilishwa kwenye mahakama hiyo bada ya saa mbili na nusu asubuhi hazitashughulikiwa.Ogoti ataamua iwapo wawili hao wataachiliwa kwa dhamana au la.

Show More

Related Articles