HabariPilipili FmPilipili FM News

Timmy Apata Pigo Mahakamani Kwa Mara Ya Pili.

Aliyekuwa gavana wa Lamu Issa Timamy amepata pigo kwa mara ya pili mfululizo.

Hii ni baada ya  mahakama ya rufaa hapa Mombasa kutupilia mbali rufaa aliyowasilisha ya kupinga ushindi wa gavana Fahim Twaha.

Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama ya rufaa Alnashir Visram.

Timmay aliwasilsiha rufaa hiyo kupinga ushindi wa gavana Fahim Twaha baada ya mahakama ya Malindi kuidhinisha ushindi wake.

Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi alikuwa ameandamana na Timamy katika mahakama hiyo.

Show More

Related Articles