HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya Mombasa yaidhinisha ushindi wa gavana wa Lamu Fahim Twaha

Ushindi wa gavana wa Lamu Fahim Twaha umedumishwa na mahakama ya rufaa huko Mombasa. Majaji watatu wakiongozwa na Alnasir Visram wamesema kesi ya kutaka kubatili ushindi wa Twaha,iliyowasilishwa na Issa Timamy haikuwa na uzito. Timamy ameagizwa kulipa shilingi milioni 6 kugharamia kesi hiyo. Ameapa hata hivyo kukata rufaa.

Show More

Related Articles