HabariPilipili FmPilipili FM News

Wananchi Katika Kaunti Yakilifi Waombwa kususia ulaji wa nyama.

Serikali ya kaunti ya kilifi kupitia idara ya afya imetoa tahadhari ya kuwepo kwa homa ya Rift Valley  katika kaunti hiyo huku wakaazi wakitakiwa kususia ulaji wa nyama.

Afisaa anayesimamia sekta ya afya tawi la Magarini  Daktari Kisa Mohammed amesema ugonjwa huo uliripotiwa wiki moja iliyopita baada ya sampuli za nyama kuchunguzwa na kuonesha chembe chembe za ugonjwa huo hivyo kupiga marufuku ulaji wa nyama.

Kwa upande wake katibu wa afya kaunti ya Kilifi Daktari Anisa Omar amesema kuwepo kwa ugonjwa huo kumeleta wasi wasi miongoni mwa wakaazi huku akiongeza kuwa sharti idara zote hata zile za usalama kushirikiana ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Haya yanajiri huku idara ya ustawi wa mifugo gatuzi ndogo la Malindi ikifunga zaidi ya vichinjio vilivyoko ndani ya kaunti ndogo za Malindi na Magarini.

Show More

Related Articles