HabariPilipili FmPilipili FM News

Hatua Ya Rais Uhuru Kutohudhuria Uzinduzi Wa Ujenzi Wa Kiwanda Cha Vyuma Kwale Yazua Hisia Mseto.

Baadhi ya wajumbe  wa bunge la kwale wanapinga uvumi uliopo kuwa rais uhuru Kenyatta hakuhudhuria uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha vyuma cha devki steel mills huko Gora eneo la Samburu kwa kuwepo kwa seneta wa Baringo Gideon Moi,  kwa madai kuwa wangeonekana pamoja ingeleta taswira kwamba anampigia debe  eneo la pwani  ili aweze kuwa  rais mwaka 2022 badala ya naibu rais Willam Ruto.

Mwakilishi wa wadi ya Puma James Dawa na mjumbe maalum katika bunge hilo Fatuma Masito wanasema seneta huyo wa Baringo ana haki ya kuwa rais na kuunga mkono miradi ya maendeleo inayofanyika humu nchini wakimpongeza kwa kuhudhuria uzinduzi huo wa devki steel mills.

Hata hivyo wanasema kwamba wanamkaribisha kikamilifu Gedion Moi  katika kaunti  ya Kwale kuomba kura za urais mwaka 2022 wakati wa siasa unapofika wakimtaja kama kiongozi aliye na maono  ya kulisongesha taifa mbele kimaendeleo .

Show More

Related Articles