HabariMilele FmSwahili

Rais na naibu wake watuma risala za rambi rambi kufuatia kifo cha mwanariadha Bett

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wametuma risala za rambi rambi kufuatia kifo cha aliyekuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita mia nne kuruka viunzi mwaka wa 2015 Nicholas Bett.Bett amekumbana na kifo chake katika ajali iliyofanyika eneo la Sochoi kaunti ya Nandi rais na naibu wake wameelezea kutamaushwa na kifo cha Bett. Rais amesema Bett atakumbkwa kwa mchango wake mkubwa katika kuinua hadhi ya taifa ulimwenguni kupitia riadha.

Show More

Related Articles