HabariMilele FmSwahili

Wauguzi kaunti ya Bomet watishia kugoma

Shughuli za matibabu kaunti ya Bomet zinatarajiwa kutatizika leo wakati wauguzi wakilenga kutimiza tishio lao la kugoma. Wauguzi hao wengi wa hospitali ya mishonari ya Tenwek, wanailaumu hospitali hiyo kwa mapendeleo, wakisema baadhi yao wametengwa katika hatua ya nyongeza ya mshahara. Wanasema hali hiyo itaaathiri utendakazi wao wakimtaka gavana wao Joyce Laboso kuingilia kati.

Show More

Related Articles