HabariMilele FmSwahiliSwahili Videos

Mwanariadha Bett aaga dunia

Aliyekuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita mia nne kuruka viunzi mwaka wa 2015 Nicholas Bett ameaga dunia .Bett amekumbana na kifo chake katika ajali iliyofanyika eneo la Sochoi kaunti ya Nandi . Alikuwa mwanariadha wa kwanza kushinda mbio za mita mia nne kuruka viunzi mwaka wa 2015.Wanariadha wenzake wakiongozwa na Isaack Barmasai wametuma risala za rambi rambi wakielezea kumpoteza mwanariadha shupavu .Kifo chake kimedhibitishwa na kamanda wa polisi Patrick Wambani .

Show More

Related Articles