HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Yaweka Mikakati Ya Kutibu Ugonjwa Wa Fistula.

Masaibu ya ugonjwa wa fistula katika kaunti ya Kilifi yanaendelea kukabiliwa vyema baada ya wizara ya afya katika kaunti hiyo kuanza kampeni kabambe ya kutibu ugonjwa huo.

Wizara hiyo inaendeleza hamasa kwa wanawake ikishirikiana na mshirika mbali mbali, hasa wale katika sehemu za vijijini ili waweze kutembelea vituo vya afya na kufanyiwa uchunguzi mapema.

Afisa msimamizi wa kitengo cha ugonjwa huo katika hospitali ya kaunti ya Kilifi Pamela Kabibu amesema kwa sasa wagonjwa 62 wamefanyiwa uchunguzi na kutibiwa na kwa sasa wanaendelea vizuri.

Pamela amewataka wanawake kuhakikisha wameshirikiana na wizara husika ili kukabiliana na ugonjwa huo ambao umeleta unyanyapaa kwa waathiriwa katika jamii

Show More

Related Articles