HabariPilipili FmPilipili FM News

Hatama Ya Rotich Na Aden Mohammed Kujulikana Leo.

Huenda mawaziri wawili wakajipata pabaya hii leo iwapo marekebisho katika ripoti ya sukari yataidhinishwa na bunge.

Hii ni baada ya kamati ya pamoja kuhusu kilimo na bishara kutarajiwa kuwasilisha ripoti hiyo ambapo iwapo bunge litaipitisha basi mawaziri Henry Rotich na Adan Mohammed huenda wakatimuliwa.

Hata hivyo kabla ya ripoti hiyo kuwasilishwa bungeni leo, kuna fununu ya mvutano ambapo inadaiwa baadhi ya wabunge wanataka kuwaokoa mawaziri hao pamoja na aliyekuwa waziri wa Kilimo Willy Bett.

Kamati hiyo ya pamoja inataka mawaziri hao kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kuhakikisha usalama wa sukari inayoingia nchini.

 

 

Show More

Related Articles