HabariPilipili FmPilipili FM News

Wawekezaji Katika Eneo Bunge La Kinango Waombwa Kutoa Nafasi Za Kazi Kwa Wananchi Katika Eneo Hilo.

Mbunge wa kinango Benjamin Tayari ametishia kuitisha  maandamano ya  kuupinga mradi mkubwa wa maji wa mwache  endapo serikali  haitabadilisha usimamizi wa mradi wa huo  kwa kile anachosema kuwa usimamizi huo haujajumuisha wenyeji wa eneo hilo la Kinango  .

Tayari ameshangazwa na jinsi usimamizi wa mradi huo  kukabidhiwa wakaazi ambao sio walengwa huku wenyeji wakisalia bila ajira, akisema  katika  uongozi wake hatokubali wakaazi wake wanyanyaswe haki zao.

Aidha ametoa changamoto kwa wawekezaji wanaowekeza katika eneo bunge lake kuhakikisha wanatoa nafasi za ajira kwa wenyeji.

Show More

Related Articles