HabariMilele FmSwahili

Waathiriwa wa shambulizi la kigaidi katika ubalozi wa Marekani hawajapata fidia miaka 20 baadaye

Miaka 20 tangu kushuhudiwa shambulizi la kigaidi katika ubalozi wa marekani humu nchini,waathiriwa wa mkasa huo wanazidi kuomba msaada. Waliofika kwa sherehe za mwaka huu katika eneo la mkasa wanadai wenzao walioathirika na shambulizi sawia Tanzania wamefidiwa wao wakisalia bila fidia.Kando na kupongeza hatua zilizopigwa na serikali kuwashughulikia waathiriwa, mkurugenzi wa kituo cha kukabili ugaidi, balozi Martin Kimani anasema ipo haja ya asasi za usalama kutekeleza vyema majukumu yao ili kulinda maisha ya wakenya.Naye balozi wa Marekani nchini Robert Godec, ameahidi msaada zaidi kwa Kenya katika vita dhidi ya ugaidi

Show More

Related Articles