Mediamax Network Limited

Bandari walenga kuvunja ubikra wa Gor Mahia kwenye KPL

Wanaforodha Bandari wanalenga kuvunja ubikra wa viongozi wa jedwali la ligi kuu humu nchini Gor Mahia .Pande hizo mbili zinapokutana hii leo ugani Mbaraki kwa mgaragazo wa ligi kuu KPL .Bandari wanaenda kwenye mtanange huu na mfumo mzuri wa kushinda katika mechi zao mbili zilizopita ; waliipiga Posta Rangers 3-0 sawia na Kariobangi Sharks . Mkufunzi wa Bandari Benard Mwalala anasema Gor Mahia ni klabu kama nyingine tu na nia yao kuu ni wapate alama tatu .Yakijiri hayo wachezaji wa Kogallo wakiongozwa na Philemon Otieno wanasisitiza lengo lao kuu ni kumaliza ligi bila ya kushindwa mechi yoyote .Kogallo wameshinda mitanange 17 na kutoka sare mara tano msimu huu . Wanaongoza jedwali na ujumla wa pointi 56 . Mechi hiyo itang’oa nanga saa tisa kamili .

……………………………………………..