HabariPilipili FmPilipili FM News

Nyumba Ya Mama Mjane Yabomolewa Kimakosa Na Askari Wa Kaunti.

Zoezi la serikali ya kaunti ya Mombasa la kubomoa na kufurusha wauzaji wa mugukaa katika maeneo ya tononoka limeiacha familia moja na kilio baada ya nyumba yao waliokua wakiishi kubomolewa kimakosa na askari hao huku wakidhani ni kibanda cha mugukaa.

Angelina,mama mjane na mwenye watoto kumi na wawili amelalamikia tukio hilo huku akisema sio mara ya kwanza kwa kitendo kama hicho kumfanyikia.

Mama huyo sasa anahofia kwamba huenda watoto wake wakajiingiza kwenye uhalifu baada ya kuvunjiwa kwa nyumba yake.

Show More

Related Articles