Mediamax Network Limited

Wanariadha wa Kenya kuwasili nchini leo jioni kutoka Nigeria

Wanariadha waliowakilisha kenya kwenye mashindano ya bara Afrika wanatarajiwa kutua katika uga wa ndege wa Jomo Kenyatta saa moja dakika 35 jioni hii leo .

Kenya imemaliza nambari moja kwenye jedwali la medali baada ya kunyakua ujumla wa medali 19; 11 za dhahabu , sita za fedha na mbili za shaba.

Walioishindia Kenya dhahabu ni Hellen Obiri (5,000m), Conseslus Kipruto (3,000m kuruka maji na viunzi), Samuel Gathimba (matembezi ya kilomita 20), Julius Yego urushaji mkuki), Elijah Manangoi (1500m), Winny Chebet (1500m), Edward Zakayo (5,000m), Beatrice Chepkoech (3,000m kuruka maji na viunzi ), Mathew Sawe (high jump), Stacey Ndiwa (10,000m) bila kusahau wanaume mbio za kupokezana vijiti .