HabariMilele FmSwahili

Wenyeji waandamana kulalamikia kutofidiwa ardhi yao Kajiado

Mamia ya wenyeji kaunti ya Kajiado wameshiriki maandamano kulalamikia kutofidiwa ardhi yao iliyotwaliwa kutoa nafasi ya mradi wa reli ya kisasa SGR.wenyeji hao wanasema kwa mwaka mmoja serikali kupitia tume ya ardhi imekuwa ikitoa hadi pasi na kuzitimiza. wakiwa wamebeba mabango, wenyeji hao wametatiza usafiri wakitaka kupewa haki yao.Nkamunu patita ni kiongozi wao ,aidha wametishia kusambaratisha mradi huo iwapo serikali haitaridhia ahadi yake.

Show More

Related Articles