HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta apongeza Emerson Mnangagwa kwa kushinda uchaguzi wa urais Zimbabwe

Rais Uhuru Kenyatta amemtumia risala za pongezi Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe baada ya kushinda uchaguzi wa urais ulioandaliwa nchini humo juma lililopita. Rais amesema ushindi wa Mnangagwa ni ishara ya imani na matarajio makubwa ya raia wa Zimbabwe katika utawala wake. Rais Kenyatta ameahidi kushirikiana na Mnangagwa katika kuboresha uhusiano wa kiuchumi na kijamii ya mataifa yote mawili. Pia rais Kenyatta amesema Kenya itafanya kazi kwa karibu na Zimbabwe katika kuafikia amani na udhabiti barani Afrika.

Show More

Related Articles