HabariPilipili FmPilipili FM News

TSC Yaitaka Serikali Kuajiri Walimu Zaidi.

Tume ya kuajiri walimu nchini TSC imeitaka serikali kutoa fedha zaidi kusimamia uajiri wa zaidi ya walimu elfu 40 wa shule za msingi.

Afisaa mkuu mtendaji wa TSC  Nancy Macharia amesema uhaba wa walimu katika shule elfu 20,665 za msingi ni takriban walimu elfu 39,574.

Amesema mwaka wa fedha wa 2017/2018 bunge lilitenga shilingi bilioni 5 za uajiri wa walimu elfu nane.

Show More

Related Articles