HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Kenyatta Kufungua Rasmi Kampuni Ya Simba Cement.

Rais uhuru Kenyatta anatarajiwa kufungua rasmi  kampuni ya simiti ya Simba ( SIMBA CEMENT )  huko Samburu eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale hapo kesho adhuhuri.

Kampuni hiyo inaaminika kupata zabuni ya kusambaza bidhaa zake katika ujenzi wa barabara nne za serikali kuu  zilizozinduliwa na rais Kenyatta mwaka jana katika kaunti hiyo.

Barabara hizo ni Kinango – Samburu, Milalani –Kilulu, Kanana –Shimoni na Lungalunga –Vanga.

Haya yanajiri kufuatia ziara ya ghafla ya rais Kenyatta katika kaunti hio kutathimini miradi ya barabara hizo siku ya Alhamisi juma lililopita.

Show More

Related Articles