HabariPilipili FmPilipili FM News

Idadi Ya Wanafunzi Waliofariki Kufuatia ya Kajali Ya Barabarani Yafikia 11.

Idadi ya waliofariki kufuatia ajali iliyohusisha basi la shule ya msingi ya ST Gabriel na lori imefikia watu 11 baada ya wanafunzi wengine wawili kufariki walipokuwa wakipokea matibabu.

Mmoja wa wanafunzi watano waliopelekwa katika hospitali ya Kenyatta alifariki jana asubuhi huku mwengine alifariki katika hospitali ya Mwingi.

Wanafunzi tisa walifariki papo hapo wakati basi lao lilipogonga lori katika daraja la Kangina kilomita moja kutoka Mwingi mjini katika barabara Thika –Garissa.

Tayari dereva wa basi hilo la shule amekamatwa kufutia ropiti ya OCPD wa Mwingi John Nyamu aliyesema dereva alikuwa akiendesha kwa kasi.

Show More

Related Articles