HabariK24 TvNEWSSwahiliVideos

Shamba la umma ladaiwa kugawiwa kampuni ya binafsi,Kahawa Sukari

Hali ya wasiwasi inazidi kutanda katika eneo la Kahawa Sukari baada ya ardhi inayoaminika kuwa ya umma na iliyotengewa shule moja ya upili kunyakuliwa na kugawanywa na kampuni moja ya ardhi katika eneo hilo.

Kulingana na wakaazi wa eneo hilo, wengi wamesalia kutishiwa kwa kuzungumzia suala hilo hadharani kwani katika miaka ya hapo awali kuna watu waliouawa kuhusiana na utata unaozunguka ardhi hiyo.

Duru kutoka tume ya ardhi nchini pia zinatilia shaka ramani iliyozinduliwa hivi majuzi na kusema haikuambatana na ya hapo awali.

 

Show More

Related Articles