HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Yamwachilia Feisal Mohammed.

Mahakama kuu mjini Mombasa  imemwachilia huru mfanyibiashara Feisal Mohammed, ambaye awali alikua amehukumiwa kifungo cha mika 20 kwa kupatikana na hatia ya ulanguzi wa pembe za ndovu za thamani ya shilingi milioni 44 manamo mwaka 2016.

Akitoa hukumu hio jaji wa mahakama kuu  mjini Mombasa Dora Chepkwonyi amesema upande wa mashtaka haukua na ushahidi wa kutosha kuthibitisha Faisal alihusika kwenye ulanguzi ,huku akisema hukumu aliyopewa hapo awali haikuambatana na sheria za nchi hii.

Uamuzi huo umejiri baada ya Feisal kukata rufaa dhidi ya hukumu ya awali

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 7 mwezi huu wa nane.

Show More

Related Articles