HabariPilipili FmPilipili FM News

Mzozo Wa Giriama Ranch Wachukua Mkondo Mpya.

Wakaazi wa Bamba gatuzi dogo la Ganze kaunti ya Kilifi wameandamana mapema leo kupinga hatua wanayodai ni kunyakuliwa kwa ardhi ya Giriama Ranch.

Wakiongozwa na katibu wa kundi  la Tairen Mijikenda , Peter Ponda, wakaazi hao wamelaani vikali hatua ya  viongozi wao wa zamani kwa kusema viongozi hao hawakushirikisha jamii walipochukua mkopo kwa benki  huo hivyo kutumia ardhi hiyo kama dhamana.

Hata hivyo wakaazi hao wameaapa kupigania haki yao kwa kila njia huku wakisema hawatarudi wala kulegeza msimamo wao wa kutetea ardhi ya mababu zao.

Ardhi hiyo yenye ekari takribani 66,000 inadaiwa kunadiwa na benki moja humu nchini baada ya viongozi wa eneo hilo kushindwa kulipa deni la benki hiyo, hivyo kutumia ardhi hiyo kama dhamana.

Show More

Related Articles