HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wanahabari wapewa siku 14 kujieleza kwa kamati ya bunge

Wanahabari wa gazeti la People Daily wana siku kumi na nne kufika mbele ya kamati ya mamlaka na fadhila bunge la kitaifa kujieleza kuhusiana na taarifa ya ufichuzi kuhusu ufisadi bungeni iliyozua kiwewe miongoni mwa wabunge.
Hii ni baada ya wanahabri hao pamoja na mhariri mkuu kuiomba kamati hiyo muda zaidi kujiandaa vyema ili kufika mbele yake.
Hata hivyo wanahabari hao wamesisitiza kwa wanakamati hao kwamba hawatashurutishwa kuelezea chimbuko lao kuhusiana na taarifa hiyo, jambo ambalo wanakamati hiyo waliafikiana.

Show More

Related Articles