HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

KNUT yasisitiza uhamisho unachangia utovu wa nidhamu shuleni

Walimu kumi na wanne nchini walioshambuliwa na wanafunzi wa shule katika mikasa ya moto iliyoshuhudiwa mapema muhula huu wamehamishwa kutoka kwenye wa shule walimokuwa huku wanafunzi waliohusika wakirudishwa nyumbani.
Haya yanajiri huku  tume ya kuajiri walimu nchini TSC ikisistiza kwamba misukosuko shuleni ni janga la kitaifa linalohitaji uchunguzi wa kitaifa huku ikipuuzilia mbali msimamo wa chama cha walimu nchini, KNUT kwamba misukosuko hiyo imesababishwa na uhamisho wa walimu na itaendelea.

Show More

Related Articles