HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Hoja kumzuia naibu Rais kuwania Urais yatupiliwa mbali bungeni

Jaribio la mbunge wa Kisumu ya kati Fred Ouda la kuwasilisha mswada wa kumzuia Naibu wa Rais William Ruto kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 limetibuka baada ya wabunge kuufutilia mbali hata kabla ya kujadiliwa.

Ouda kwenye mswada wake alidai nafasi ya rais na naibu wake ni moja hivyo basi tayari Ruto amehudumu katika wadhifa wa urais kwa mihula miwili.

Hata hivyo wabunge wamesema mswada huo wa Ouda hauna msingi wowote wa kisheria.

Show More

Related Articles