HabariPilipili FmPilipili FM News

Omar Mwinyi Kwenda Jela Miaka Minne.

Mbunge wa changamwe Omar Mwinyi apatikana na makosa ya kuwapiga na kuwajeruhi maafisa wa 2 wa polisi wakati wa kura za mchujo za chama cha ODM mwezi april mwaka wa 2017.

Hakimu mkuu Evans Makori amesema mbunge huyo alihusika pakubwa katika kuwajeruhi polisi hao kwa kuwa alishindwa kuwazuia wafuasi wake waliojeruhi maafisa hao.

Mahakama imempata na hatia Omar Mwinyi na kumfunga kifungo cha miaka nne gerezani au faini ya shilingi 1,000,000.

Show More

Related Articles