HabariPilipili FmPilipili FM News

Hali Mbaya Ya Anga Yatatiza Usafiri Wa Ndege JKIA.

Shughuli za usafiri katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi zimetizika kufuatia hali mbaya ya hewa.

Baadhi ya ndege ambazo zilipangiwa kutua katika uwanja huo mapema leo asubuhi zilielekezwa katika viwanja vingine ikiwemo uwanja wa ndege wa Moi hapa Mombasa.

Katika taarifa kupitia mtandao wa Twitter, shirika la KENYA Airways limesema ndege hizo zilitatizwa kutua kufuatia ukungu.

Show More

Related Articles